Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sare ya Stars yamvuruga Kocha Zambia

Stars 70Tc.jpeg Sare ya Stars yamvuruga Kocha Zambia

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Zambia, Avram Grant alibaki amefura kwa hasira baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Tanzania juzi katika mechi ya Kundi F la fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Kikosi cha Grant kilifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho wa mchezo huo na kuiwezesha Zambia kupata pointi moja, lakini hakufurahishwa na timu yake ilivyocheza licha ya kukubali kwamba Tanzania ilikuwa vizuri sana katika mechi hiyo.

“Ni matokeo yanayofadhaisha. Tulijua haitakuwa mechi rahisi baada ya kuishuhudia Tanzania ilivyocheza dhidi ya Morocco. Ni kweli kwamba tulianza vyema lakini tukaruhusu bao mapema na jambo hilo likabadili mbinu zetu hasa baada ya kadi nyekundu,” alisema.

Kocha huyo ambaye aliifikisha timu katika fainali ya AFCON 2015 alikiri kwamba kucheza na watu 10 kwa muda mrefu wa mchezo sio jambo rahisi na lilikuwa na athari kubwa kwao.

“Ni ngumu kucheza mkiwa na watu 10 uwanjani. Lakini nina furaha na vijana wangu kwa walivyopambana (baada ya nahodha kutolewa kwa kadi ya pili ya njano). Walijitoa kwa kila kitu hadi kusawazisha.”

Zambia imebakisha mechi moja ya kucheza dhidi ya timu iliyofika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 kule Qatar na ambayo inapewa nafasi kutwaa taji hili, Morocco.

Grant anaa mini timu yake itacharuka na kushinda dhidi ya Simba wa Atlas kesho.

“Tayari tunajua kwamba Morocco ni timu kubwa lakini hatuwaogopi. Tutawakabili na tunatumaini tutacheza kwa kiwango bora. Ni lazima tuonyeshe uwezo.”

MSIKIE MOROCCO

Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, alisema timu yake ilicheza vyema, lakini ikapoteza umakini katika dakika 10 za mwisho na hicho ndicho kilichowaharibia.

Alisema wanajua wana mechi ngumu ijayo dhidi ya DR Congo lakini watapambana ili kupata ushindi kesho saa 5:00 usiku.

Mfungaji wa bao la Tanzania, Simon Msuva, ambaye sasa amefikisha mabao 22 kwa timu ya Taifa Stars (sawa na Mbwana Samatta wakiwa mabao matatu nyuma ya kinara wa muda wote Mrisho Ngassa mwenye 25), alisema wanayo nafasi ya kushinda mechi ya mwisho na hata kufuzu 16-Bora kwa mara ya kwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live