Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sankara Karamoko ndiye kinara wa mabao CAFCL mpaka sasa

Karamoko Sankara Sankara Karamoko ndiye kinara wa mabao CAFCL mpaka sasa

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sankara Karamoko, kutoka Côte d'Ivoire, ndiye top scorer wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika mpaka sasa baada ya mzunguko wa tatu wa hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Sankara (20) anayekipiga ASEC Mimosas amefunga mabao matatu kwa dakika 84 tu alizozipata kucheza kwenye michuano hiyo msimu huu.

Anatajwa kama mmoja wa washambuliaji hatari sana ambao huenda wakatesa Bara la Afrika miaka ya hivi karibuni baada ya kuondoka akina Mo Salah na Sadio Mane.

Sankara amekuwa akiitwa mara nyingi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast.

Mkataba wake na ASEC Mimosas unamalizika Juni, 2025 ambapo Yanga SC wanatajwa kuwa wameshatupa ndoano yao kumnasa fundi huyo huku thamani yake ni Milioni 807 Tsh sokoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live