Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sanga amvaa Rage "Hii sio Ligi ya Mbuzi"

Sanga Rage Sanga na Rage

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Makete na Mwanachama wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Festo Richard Sanga, ameonesha kukerwa na kauli iliyotolewa na mdau wa soka nchini Ismail Aden Rage, alipohojiwa na vyombo vya habari jana Jumapili (Machi 13).

Rage ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Simba SC alitoa kauli ya kuidharau Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuiita Ligi ya Mbuzi, jambo ambalo limepingwa vikali na Sanga.

“Sisi tumebakisha mechi moja, tukishinda tunasonga mbele, hilo kombe lingine la mbuzi tunawaachia,” alisema Rage.

Katika kuonesha kukerwa kwake na kauli hiyo ya Rage, Sanga ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kueleza: “Ligi Kuu Tanzania bara sio LIGI YA MBUZI, hii ndio ligi inayowafanya Simba wacheze CCL na shirikisho.

“Hii ndio ligi ambayo serikali na sekta binafsi wamewekeza fedha na kuajili maelfu ya watanzania. Hii ndio ligi ilikufanya RAGE uitwe RAGE nchi hii, TUJIZUIE KUROPOKA, PERIOD,” alisema Sanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live