Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sanga: Mo Dewji anataka tumpigie magoti

Sanga Dejwi Sanga, Mo Dewji.

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku moja baada ya Mwanachana na Shabiki wa Simba SC Ally Mikoi ‘Kisugu’ kumtaka Mbunge wa Makete Festo Sanga kuacha kuizungumzia Simba SC vibaya, Mbunge huyo ameibuka na kumjibu Kisugu.

Mbunge Sanga amesema haishambulii Simba SC kama inavyozemwa na wengi na kuongeza ni mapenzi yake dhidi ya timu hiyo.

“Kwa miaka takribani mitano soka letu limekuwa na ushiriki wa vilabu vyetu kwenye michuano ya kimataifa umekuwa mkubwa sana, maana yek watu wanakuangalia kwa jicho la karibu sana, inapofika timu inaanza kupambana ili isalimike kubaki Champions League, tunaishusha heshima timu yetu.

“Wamemuondoa kocha kwa kisingizio kuwa ana matatizo ya kifamilia lakini Watanzania na wadau wa soka wanahoji hata benchi la ufundi nao wana tatizo la kifamilia? Tunajua wanajaribu kuficha ukweli, tuseme ukweli wala wasiseme mbunge wa Makete anaishambulia Simba, hatuishambulii, lazima umwambie daktari ukweli ili aweze kukutibu.

“Kupata matokeo na uongozi ni vitu viwili vinavyoendana, ukiwa na uongozi mzuri unaweza kupata matokeo mazuri zaidi au usipate matokeo. Viongozi wa Simba wakiwa imara, funding ikiwa nzuri, mwekezaji akiwa stable, moja kwa moja tutaona matokeo uwanjani. Usajili utakuwa mzuri na mwenendo mzuri wa klabu.

“Siku ambayo Mo alisema anaachana na Simba anakuwa rais wa heshima ndipo Simba ilianza kutetereka, maana yake mwekezaji anajua anachokifanya, labda tukampigie magoti atoe fedha ili Simba ipate matokeo, ama anataka tuandamane tuseme bila yeye timu haiwezi kwenda, hapana tusifike huko, Simba ni kubwa kuliko mtu yeyote yule.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live