Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sane auomba uongozi wa Bayern wasimfukuze Mane

Leroy Sane Bayern Munich Sadio Sane auomba uongozi wa Bayern wasimfukuze Mane

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Bayern Munich, Leroy Sane ameuomba Uongozi wa timu hiyo kutomfukuza, Sadio Mane licha ya kuchezea kichapo kutoka kwa nyota huyo wa zamani wa Liverpool.

Leroy Sane alipigwa ngumi ya uso na Mane baada ya kupoteza mchezo wao mbele ya Manchester City hatua ya robo fainali ya Champions League kwenye uwanja wa Etihad siku ya Jumanne.

Winga huyo raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 31, alisimamishwa na Bayern siku ya Alhamisi baada ya yeye na Leroy Sane kukaa kikao na uongozi wa timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live