Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sancho kuwekwa kitako Man United

Jadon Sancho Saga Jadon Sancho

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imepanga kukutana na Jadon Sancho ili kumpasha ukweli juu ya mwelekeo wa maisha yake ya baadaye kwenye kikosi.

Winga huyo amekuwa na msimu wenye mapito mengi. Baada ya kukutana na wakati mgumu huko Man United na kuweka benchi na Kocha Erik ten Hag, alihama kwa mkopo kwenda Borussia Dortmund kwenye dirisha la Januari na kuonyesha kiwango bora kabisa.

Sancho, ambaye mkataba wake huko Man United utafika tamati 2026, alirudi kwenye ubora wake na kuisaidia Dortmund kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, walipochapwa 2-0 na Real Madrid, Jumamosi iliyopita. Sasa, hafahamu nini kitafuata kwenye maisha yake.

Dortmund ipo tayari kumbakiza na Sancho mwenyewe hayupo tayari kurudi Man United endapo kama Ten Hag ataendelea kuwa kocha.

Lakini, mabosi wakubwa wa Man United wamepanga kujadiliana na Sancho juu ya jambo hilo ili kupata suluhu ya nini kifanyike.

Ripoti zinafichua kwamba mkurugenzi wa ufundi, Jason Wilcox na mkurugenzi wa makubaliano wa soka Matt Hargreaves atafanya watazungumza na wawakilishi wa Sancho kabla ya pre-season kuanza. Wachezaji wote watahitajika kurudi kujiunga na timu mwezi ujao kabla ya mechi yao ya kwanza ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya itakayofanyika Julai 15.

Dortmundinamtaka Sancho, lakini kutokana na bei anayouzwa mchezaji huyo na mshahara anaolipwa, miamba hiyo ya Bundesliga inachotaka kukifanya ni kumnyakua tena kwa mkopo winga huyo wa England.

Kocha wa Dortmund, Edin Terzic alisema: “Kwa miezi sita iliyopita, Jadon amekuwa bora sana kwetu. Sawa, ilimchukua muda kurudi kwenye ubora wake. Lakini, ulikuwa ni ubora ambao unafahamu kabisa unakwenda kuongeza kitu kwenye timu yetu. Aliboresha kiwango chake na wale wanaomzunguka.”

Sancho alitoa ujumbe wa kuwaaga mashabiki wa Dortmund baada ya muda wake wa mkopo kufika mwisho.

Chanzo: Mwanaspoti