Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sancho apigwa marufuku kutumia Mgahawa wa Timu

Jadon Sancho Jadon Sancho

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sakata la Mchezaji wa United Jadon Sancho na klabu yake linaendelea na sasa mchezaji Huyu apigwa marufuku kutumia mgahawa .

Sancho haruhusiwi kabisa kutumia mgahawa wa kikosi cha kwanza cha United. Marufuku hiyo inahusu pindi anapokuwa kwenye Viwanja vya Mazoezi vya Carrington, ikiwa ni mwendelezo wa adhabu aliyopewa kutoka na kuchapisha andiko ambalo lilipinga maneno ya meneja wake Erik ten Hag

Tangu aondolewe kikosini mchezaji Huyu amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Vijana ambapo hata wakati wa chakula hatakiwi kutumia Mgahawa unaotumiwa na timu ya vijana.

Inadaiwa Sancho alikuwa na tabia ya kuchelewa Mazoezini mara kwa mara na alishindwa kufikia viwango vinavyohitajika na kocha wake, ili arejee kikosini Sancho amepewa sharti la kuomba radhi jambo ambalo hajafanya mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live