Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sancho akubaliana na Paris St-Germain

Sanchoooooooooo Jadon Sancho

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Paris St-Germain imeripotiwa kufikia makubaliano na wawakilishi wa winga wa Manchester United, Jadon Sancho kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili la usajili barani Ulaya.

Mbali ya kufikia makubaliano na Sancho kwenye masuala mbalimbali ikiwemo mshahara na bonasi ya usajili, timu hiyo itatakiwa pia kufikia makubaliano na Manchester United inayotaka kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni ili kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa England aliyekuwa akikipiga Dortmund dirisha lililopita kwa mkopo.

Awali ilielezwa Man United haikuwa na mpango wa kumuuza nyota huyo baada ya kumaliza mgogoro wake na kocha Erik ten Hag, lakini mambo ni kama yamebadilika. Mkataba wa Sancho unatarajiwa kumalizika 2027 na msimu uliopita alicheza mechi 24 za michuano yote na kufunga mabao matatu. Timu nyingi zilihusishwa kutaka kumsajili staa huyo lakini kabla ya kuripotiwa kwamba mgogoro wake na kocha wa Mashetani Wekundu umemalizika.

Wakati huo huo Chelsea imefanya mawasiliano na wawakilishi wa mshambuliaji wa Juventus na Italia, Federico Chiesa, 26, kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili na inaelezwa kwamba wanakutana na upinzani mkali kutoka Tottenham Hotspur ambayo pia inahitaji saini yake. Chiesa ambaye msimu uliopita alifunga mabao 10 katika mechi 35 za michuano yote, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2025.

MANCHESTER United imefikia makubaliano na Bayern Munich juu ya kumsajili beki wa kulia wa timu hiyo, Noassair Mazraoui ambapo itatakiwa kutoa ada ya usajili inayofikia Pauni 15 milioni. Mabosi wa Manchester United wanataka kumsajili nyota huyo ili akawe mbadala wa Aaron Wan-Bissaka anayedaiwa kuwa katika mpango wa kutua Galatasaray.

ASTON Villa imewasilisha ofa Manchester City kwa ajili ya kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo na timu ya taifa ya England, Kalvin Phillips katika dirisha hili. Phillips ambaye ana mkataba na Man City hadi 2027, anadaiwa kwamba hana mpango wa kuendelea kusalia katika timu hiyo kwa sababu haoni kama yupo katika mipango ya msimu ujao.

MABOSI wa Barcelona hawana mpango wa kumsajili beki wa kulia wa Manchester City, Joao Cancelo, 30, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika timu hiyo. Cancelo, 30, Man City ipo tayari kumwachia lakini kwa kiasi cha pesa kisichopungua Pauni 25 milioni ambacho Barca inaona ni kikubwa. Mkataba wake unamalizika 2027.

ARSENAL inadaiwa kuwa katika hatua nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres katika dirisha hili licha ya Liverpool kudaiwa kuingila dili hilo. Staa huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 26, anawindwa na vigogo wengi Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita ambapo alicheza mechi 50.

WEST Ham United ipo tayari kulipa Pauni 29.5 milioni kwa ajili ya kumsajili kiungo wa AS Monaco, Youssouf Fofana, 25, katika dirisha hili baada ya kufanya mazungumzo ya muda mrefu na wawakilishi wa mchezaji na mabosi wa Monaco. Fofana mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2025 na amekuwa wa moto kwelikweli kikosini.

EVERTON imefikia makubaliano na Olympiqiue Lyon kwa ajili ya kumsajili beki wa timu hiyo na Jamhuri ya Ireland, Jake O’Brien, katika dirisha hili kwa ada ya uhamisho inayodaiwa kufikia Pauni 22 milioni. Mabosi wa Everton walianza mazungumzo na wa Lyon juu ya staa huyo mwenye umri wa miaka 23, kwa muda mrefu. Mkataba wake unamalizika 2027.

Chanzo: Mwanaspoti