Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sancho aende, Malen aje Man United

Jadon Sancho Sancho aende, Malen aje Man United

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United inataka kuwashawishi Borussia Dortmund wafanye biashara ya kubadilishana wachezaji na wao wawape Jadon Sancho jumla ili wamchukue Mdachi Donyell Malen.

Sancho alijiunga na Dortmund kwa mkopo dirisha la Januari baada ya kutibuana na Kocha Erik ten Hag huko Man United na kinachoonekana ni mchezaji huyo hataki kurudi kucheza Old Trafford kama kocha huyo Mdachi ataendelea kubaki kwenye kikosi hicho.

Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la Bild, Man United inavutiwa na mpango wa kubadilishana wachezaji.

Hata hivyo, juu ya kumpata Malen, mchezaji huyo amekuwa kwenye rada za Arsenal na Liverpool pia, zikihitaji huduma yake kutokana na kufanya vizuri huko Ujerumani.

Malen, 25, amekuwa kwenye kiwango bora, akifunga mabao 13 na kuasisti mara tano katika mechi 33 za michuano yote aliyocheza kwenye kikosi hicho cha Dortmund msimu huu.

Sancho, 23, ambaye amefunga mara moja na kuasisti mara moja pia kwenye mechi tisa alizocheza kwenye Bundesliga hii ni mara yake ya pili kuitumikia timu hiyo yenye jezi za rangi nyeusi na njano.

Mkataba wa Sancho huko Man United utafika tamati kwenye majira ya kiangazi 2026, huku miamba hiyo ya Old Trafford ikiwa na kipengele cha kumwongezea mwaka zaidi endapo ikihitaji kufanya hivyo.

Chanzo: Mwanaspoti