Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sanamu la Wenger lazinduliwa Arsenal

Wenger Arsenal Sanamu la Wenger lazinduliwa Arsenal

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Arsenal imezindua sanamu la Arsene Wenger ambaye amedumu kwa kuifundisha klabu hiyo kwa muda wa miaka 22 na limewekwa nje ya Uwanja wa Emirates. Wenger anatajwa kuwa miongoni mwa makocha bora wa Ligi Kuu England kwani aliiongoza Arsenal jumla ya mechi 1,235 na kuipa mataji matano ya Kombe la FA.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 73 alieuliwa kuwa kocha wa Arsenal tangu mwaka 1996 na akawa kocha wa kigeni kushinda taji la ligi na FA msimu wake wa kwanza.

Huo ndio ukawa mwanzo wa mafanikio ya Wenger na amebeba mataji mengine ya ligi msimu wa 2001-2002 na 2003 na 2004 na kuweka rekodi ya kubeba ubingwa bila kufungwa mechi 49.

Sasa kutokana na mafanikio hayo klabu hiyo ilimjengea sanamu Wenger lenye urefu wa mita 3.2 nje ya Uwanja wa Emirates. Sanamu hilo limejengwa na Jum Guy na kuzinduliwa wiki iliyopita ilichukua mwaka mmoja kukamilisha. Kocha wa sasa wa Arsena, Mikel Arteta alisifia ubunifu huo akidai ni jambo la heshima kwa mkongwe huyo kujengewa sanamu kutokana na mambo makubwa aliyofanya.

"Sanamu hilo litakuwa kama ukumbusho na litakuwa nje ya uwanja maisha yote, hakika ni heshima kubwa na amestahili. Nilipostaafu kucheza soka nilimfuata na kumuuliza kama nitafiti nikijiingiza katika masuala ya ukocha na kunibariki kwamba naweza sikuwa na mawazo hayo kwa wakati huo."

Wenger ataungana na malejendi wengine waliojengewa sanamu kama Tony Adams, Dennis Bergkamp, Herbert Chapman, Ken Friar na Thiery Henry.

Arteta akamaliza kwa kusema alijifunza mambo mengi kutoka kwa Wenger: "Alikuwa ana upendo na klabu kwa jinsi alivyokuwa akiitetea, alikuwa mwaminifu sana ndio mambo makubwa ambayo nimejifunza kwake."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: