Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sanamu la Perez liwekwe wapi pale Real Madrid?

Perez Pic Data Rais wa Real Madrid, Florentino Perez

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Lorenzo Sanz anagombea kiti cha Urais, Real Madrid pale mwaka 2000 aliamini Real Madrid kuchukua ubingwa wa UEFA 1998 na 2000 ingemsaidia kuwa Rais wa Real Madrid kwa awamu nyingine.

Upande wa pili, injinia, mfanyabiashara na mwanasiasa mwenye net worth ya dola za kimarekani bilioni 2.5 kwa mujibu wa Forbes, Florentino Perez Rodriguez alisema kuwa atamleta Luis Figo pale Madrid kutokea Barca.

Sanz alipigwa chini na Perez.

Huyu ndio muasisi wa Galactico (exceptionally) pale Madrid, Luis Figo, Zizzou, CR7, Karim Benzema, Kaka Ricardo, Xabi Alonso, James Rodriguez, Gareth Bale, James Rodriguez na wengine unaowajua, ni magalactico ambao aliwataka Perez na akawapata.

Ukiachana na kununua magalactico, Sasa hivi yeye ndio anatengeneza magalactico, akina Fede, Vini, Rodrygo, Endrick, Camavinga na wengine wanaelekea huko.

Kwangu huyu ni baada ya Santiago Bernabeu De Yeste, Rais wa zamani wa Real Madrid.

Baada ya Santiago Bernabeu De Yeste, Don Perez ni Rais bora wa muda wote kwenye vilabu.

Sijui sanamu lake litawekwa wapi huyu mzee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live