Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samuel Eto'o ashinda Urais Cameroon

Etoo Rais mpya wa Shirikisho la Mpira Cameroon

Sun, 12 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Kandanda barani Afrika na Cameroon Samuel Eto’o amechaguliwa rasmi kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Cameroon (FECAFOOT).

Uchaguzi huo umefanyika Jumamosi Disemba 11, 2021 ambapo Samuel Etoo amepata kura 41 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidou Mbombo Njoya ambaye amepata kura 31.

Mshindi huyo mara nne wa tuzo ya mchezaji bora Afrika alianza kwenye kinyang’anyiro cha wagombea saba kabla ya wapinzani watano kujiweka kando na upinzani kusalia kwa wawili hao.

Kazi kubwa ambayo ataanza nayo Samuel Etoo itakuwa ni kuandaa fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2022 ambapo taifa la Cameroon litakuwa mwenyeji.

Wakati wa mchakato wa kutangaza nia ya kugombea urais nchini humo, Eto'o alishawishiwa kujitoa huku akiahidiwa kupewa nafasi ya Makamu wa Rais.

Eto'o ameahidi kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Shirikisho hilo ili tu kuokoa mpira wa miguu.

Mbali na hilo mchezaji huyo wa Zamani aliepata mafanikio na Barcelona, Inter Milan na Chelsea ameahidi kujenga viwanja takribani 10 wakati wa uongozi wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live