Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samuel Eto'o: Cameroon itabeba Kombe la Dunia

Samuel Etoo 1 Rais wa Shrikisho la Soka Cameroon, Samuel Eto'o

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati zikiwa zimebaki siku 11 tu kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia, Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon, Samuel Etoo anaamini watashinda kombe la Dunia ingawa hawapewi nafasi kubwa.

Akizungumza kuelekea kuanza kwa michuano hiyo Etoo amesema;

"Tuna uwezo wa kushinda Kombe la Dunia, hakuna haja ya kutisha tunahitaji zaidi maandalizi mazuri na mawazo thabiti kama Milan walivyofanya mwaka 2010".

Michuano ya Kombe la Dunia itaanza Novemba 20 mwaka huu, huku Cameroon wakiwa chini ya gwiji wa zamani wa Timu hiyo Regobert Song.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live