Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia achangia Sh500 milioni timu za Taifa

Rais Samia Suluhu Leo Mei 13 Rais Samia Suluhu Hassan

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Rais Samia Suluhu Hassan amechangia Sh500 milioni katika harambee ya kuzichangia timu za Taifa inayoendelea hapa Dar es Salaam.

Akizungumza moja kwa moja kwa njia ya mtandao na wadau wa michezo waliojitokeza katika harambee hiyo, Rais Samia amesema kuwa mchango huo ni mwendelezo wa juhudi za serikali kukuza michezo.

"Michezo pia ni gharama ndugu zangu. Serikali imejitahidi, tumehamasisha, timu zetu zinasonga mbele lakini tumefika mahala tuna uchache wa bajeti. Wito wangu na ombi langu kwenu Watanzania wenzangu, tuchangie timu zetu ili ziende kuwakilisha jina la Tanzania.

"Kwa kuanzia mimi na marafiki zangu wameniahidi kwa kusema tutachangia Sh500 milioni. Niwaombe sana shughuli iende vizuri, niwaombe ndugu zangu tuendelee na michango," amesema Rais Samia.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ndiye anaongoza harambee hiyo, alisema kuwa lengo kuu ni kukusanya kiasi cha Sh10 bilioni ambacho kitagawanywa kwa timu za taifa za michezo tofauti.

Chanzo: Mwanaspoti