Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sambou kuikosa Simba SC Jumamosi

Image 318.png Sambou kuikosa Simba SC Jumamosi

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: Dar24

Mshambuliaji wa Mabingwa wa soka Barani Afrika Wydad Casablanca Bouly Junior Sambou ameenguliwa katika kikosi cha miamba hiyo ya Casablanca-Morocco kitakachoikabili Simba SC ya Tanzania katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali, Ligi ya Mabingwa.

Simba SC itakuwa mgeni wa mchezo huo utakaopigwa Jumamosi (April 22), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kuanzia saa kumi jioni.

Sambou mwenye umri wa miaka 24 atakosekana Katika mchezo huo kutokana na kuwa na Kadi tatu za Njano.

Hata hivyo Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa klabuni hapo mwaka 2022 akitokea ASC Jaraaf ya nchini kwao Senegal, anatarajiwa kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili dhidi ya Simba SC, mjini Casablanca mwishoni mwa juma lijalo.

Tayari kikosi cha Wydad Casablanca kimeshawasili jijini Dar es salaam mapema leo Jumatano (April 19) majira ya asubuhi, kwa ajili ya kukabili Simba SC.

Chanzo: Dar24