Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta uso kwa uso na Man United

Mbwana Samatta Debut Samatta uso kwa uso na Man United

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa kimataifa wa Tanzania na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta mwezi huu anatajiwa kuanza kucheza mechi za michuano ya Ligi ya UEFA Europa League akiwa na klabu ya PAOK ya Ugiriki, huku akitarajiwa kuja kukutana uso kwa uso Man United, Novemba 7 mwaka huu.

Katika droo ya michuano hiyo inayoendeshwa kwa mtindo wa ligi tofauti na ilivyokuwa zamani iipochezwa kwa makundi, iliyofanyika jijini Monaco, Ufaransa, PAOK ya Samatta ikipangwa chungu namba mbili na Lyon, Fenerbahce, Real Sociedad, Braga, AZ Alkmar, Olympiacias, M.Tel Aviv na Ferencvaros.

Hata hivyo, Samatta amekuwa hana nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza, Mara ya mwisho Samatta kuonekana uwanjani ilikuwa Julai 31 katika mechi ya Ligi dhidi ya Borac Banja Luka akikaa benchi, huku timu yake imecheza mechi nane za mashindano mbalimbali lakini Mtanzania huyo hakuwepo hata benchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live