Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta kutua leo kuongeza nguvu Stars

Samatta Stars?fit=640%2C360&ssl=1 Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' anatarajiwa kuwasili leo majira saa tano usiku  nao shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) waomba sapoti.

Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa nchi Ubelgiji katika klabu ya Royal Antwerp anatarajia kuwasili leo nchini kujiunga na kambi ya Stars kwa maandalizi ya mchezo wao dhidi ya DR Congo Novemba 11 katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Meneja wa Taifa Stars Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kuwa wachezaji 26 tayari wapo kambini huku nahodha wao akitarajiwa kuwasili leo saa tano za usiku.

"Hali ya wachezaji ni nzuri na tunaendelea na mazoezi huku wachezaji 26 tayari wapo kambini na leo saa tano usiku tunatarajia kuwasili kwa nahodha wetu Samatta ili kukamilisha idadi ya wachezaji 27"

""Kila mchezaji anajua umuhimu wa mechi hii na wanaonyesha kuwa na kiu ya kufanya vizuri hapa nyumbani kwani wanajua wana deni kubwa kwa Watanzania"

Kwa upande wa shrikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kupitia katibu wao Wilfred Kidao wameomba Watanzania kuja kwa wingi kuisapoti timu yao.

"Kwa muda mrefu hatujawahi kufikia hatua kama hii hivyo timu yetu inaonyesha kua na matumaini ya kufika mbali hivyo Watanzania waje kuisapoti timu yao"

"Pia tumeona juhudi za Serikali kuipa nguvu Taifa stars na hii imeonekana wazi baada ya Waziri Mkuu kuitisha vikao pamoja na wadua kuhakikisha tunafanya vizuri"

"Lakini kikubwa ni kua Watanzania watakaokuja kuutazama mchezo basi waje huku wakifata protoko za uviko-19 na hata hivyo tumeweka viingilio rafiki hivyo tunaomba tuisapoti na tushirikiane kwa pamoja kuipa hamasa timu yetu" Alisema Kidao

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz