Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta kubeba Ubingwa Ubelgiji ni suala la muda tu

Skysports Mbwana Samatta 4893444 Mbwana Samatta

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Captain wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye ni mshambuliaji wa kikosi cha KRC Genk, juzi alitupia na kutoa assist kwenye ushindi ambao umeifanya timu hiyo kukaribia kuchukua ubingwa wa ligi ya Ubelgiji.

Ushindi huo unaifanya Genk iendelee kusalia kileleni na imebakiza mechi moja tu kukamilisha msimu.

Baada ya mechi hiyo timu nne za juu ikiwepo Genk, Saint Gilloise, Royal Antwerp zitaenda kwenye mchujo ya ubingwa huku wakisubiri kati ya Club Brugge au Gent kuingia kwa sababu wote wana pointi 56.

Katika Playoff hiyo, timu nne ambazo zinacheza zitagawanywa pointi zake mara mbili ambazo walimaliza nazo kwenye Ligi Kuu kisha ndio wataanza kucheza mechi za mchujo ambazo zipo sita kisha mwenye pointi nyingi ndio bingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live