Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta awaharibia mabosi wake Ulaya

Samatta Goal Mbwana Samatta akidhibitiwa na walizi wa Fenerbahce

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa jana kulikuwa na michezo ya kombe la Uropa(UEFA UROPA LEAGUE)na moja kati ya michezo hiyo ilikua ni mchezo kati ya Fenerbahce dhidi ya Royal Antwerp.

Katika mchezo huo wa Kundi D uliopigwa nchini Uturuki uliisha kwa sare ya magoli 2-2.

Mtanzania Mbwana Samatta ambae anaichezea Royal Antwerp kwa mkopo akitokea Fenerbahce, amefunga moja kati ya magoli ya Royal Antwerp na kutibua mipango ya waajiri wake.

Goli jingine la Royal antwerp limefungwa na P. Gerkens 62' huku yale ya Fenerbahce, yakifungwa na E. Valencia aliefunga magoli yote mawili, moja likiwa kwa mkwaju wa Penati.

Royal Antwerp inashika mkia katika kundi D, ikiwa na alama moja tu baada ya kucheza michezo mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live