Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta avalishwa mabomu PAOK

Mbwana Samatta Debut Samatta avalishwa mabomu PAOK

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta atakuwa mzigoni keshokutwa, Jumatano kupigania nafasi ya kucheza fainali yake ya kwanza huko Ugiriki kwa kuliongoza chama lake, PAOK Thessaloniki katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya kombe la ligi nchini humo dhidi ya Panathinaikos.

Samatta ambaye alikosekana kwenye kikosi hicho kwa wiki kadhaa kutokana na majukumu ya kitaifa akiwa na Taifa Stars kwenye fainali za mataifa ya Afrika 2023 ambazo kilele chake ilikuwa jana, Jumapili huko Ivory Coast, ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa PAOK Thessaloniki.

PAOK ambao wanaonekana kuwa kwenye kiwango bora kwenye michuano ya ndani huko Ugiriki hadi Ulaya, wataanzia nyumbani kwenye uwanja wao wa Toumba kabla ya kurudiana Jumatano ijayo, Februari 21 na mashindi wa jumla atacheza fainali na Panaitolikos  au Aris.

Kocha wa PAOK, Razvan Lucescu alifurahishwa na urejeo wa Samatta kikosini na aliweka wazi kwenye moja ya mahojiano yake kuwa hiki ni kipindi ambacho anatamani kuwa na wachezaji wake wote wakiwa fiti.

“Hatutakiwi kupoteza mwelekeo, tunatakiwa kuwa kamili, tupambane kama timu kuhakikisha tunaweka historia kwa pamoja, Ally (Mbwana) amerejea hivyo ni jambo jema kwetu,” alisema kocha huyo ambaye alimtumia kwenye mchezo uliopita kwenye ligi ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya Atromitos.

Uzoefu wa Samatta ni miongoni mwa vitu ambavyo vimekuwa vikiisaidia PAOK msimu huu kwenye mashindano mbalimbali pamoja na kwamba kasi ya upachikaji mabao ya mshambuliaji huyo inaonekana kupungua amekuwa kiongozi mzuri kwenye idara ya ushambuliaji ya chama hilo.

Lucescu anajua namna nzuri ya kumtumia Samatta, kuna mechi ambazo amekuwa akisimama kama mshambuliaji wa mwisho na nyingine huanzia benchi kwa lengo la kuusoma mchezo kisha huingia kwa lengo la kuleta mabadiliko na katika hilo kocha huyo amekuwa akifanikiwa.

Samatta menye miaka 31, amepachika mabao mawili na kutoa asisti tatu kwenye michezo 15 ya ligi aliyocheza lakini amehusika kwenye utengenezaji wa mashambulizi hatari saba ambayo yalizaa mabao huo ndio uhatari mwingine wa nahodha huyo wa Stars.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live