Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta atua Stars na matumaini kibao

30d4e1afa45f67d101aea3dde3cf77d1 Samatta atua Stars na matumaini kibao

Wed, 7 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema ana imani watafanya vizuri katika mechi ya kimataifa ya kirafi ki dhidi ya Burundi itakayochezwa mwishoni mwa wiki hii.

Mshambuliaji huyo anayecheza soka la kulipwa Fenerbahce ya Uturuki aliwasili Dar es Salaam jana alfajiri kujiunga na wenzake katika kambi maalumu ya maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa Jumapili ya wiki hii.

Akizungumza baada ya kutua, mchezaji huyo alisema alikiona kikosi cha Taifa Stars kilichotangazwa hivyo anaamini watapata matokeo mazuri.

“Naamini wachezaji walioitwa tutapata matokeo mazuri, kwa sababu niliona majina ya wachezaji, wengi wanaonekana kuwa imara,”alisema.

Taifa Stars na Burundi zilikutana mwaka jana mara mbili katika michuano ya kufuzu Kombe la dunia na zote kutoka sare ya bao 1-1.

Mbali na Samatta, wengine walioitwa Stars ni Simon Msuva, Ditram Nchimbi, Metacha Mnata, Aishi Manula, David Kissu, Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Mohamed Hussein, Brayson David, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Sebo na Dikson Job. Wengine ni Idd Mobby, Jonas Mkude, Himid Mao, Feisal Salum, Ally Msengi, John Bocco, Mzamiru Yassin, Iddy Nado, Thomas Ulimwengu, Nickson Kibabage, Said Hamis ‘Ndemla’ na Salum Abubakar.

Chanzo: habarileo.co.tz