Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta amwachia msala Kocha Amrouche

Video Archive
Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amesema kuwa ni wakati sahihi wa benchi la ufundi chini ya kocha Adel Amrouche kufanya homework yao vizuri na kupanga mikakati namna ya kupata matokeo kwenye michezo yao miwili ya AFCON iliyosalia.

Akizungumzia hilo baada ya mchezo huo kumalizika na Stars kuchabangwa bao 3-0 dhidi ya Morocco, katika Uwanja wa Laurent Pokou nchini Ivory Coasta yanakochezwa mashindano ya AFCON 2023.

"Tunafahamu tuna mechi tatu za kucheza kwenye kundi letu, kwa hiyo ni muda wa benchi la ufundi kuangalia mechi ya Zambia na Congo jinsi gani tunaweza kupata matokeo kwa sababu ndio wapinzani ambao tutacheza nao.

"Ni nafasi nzuri ya kuangalia mapungufu yao na ubora wao uko wapi ili kutengeneza timu kwa ajili ya mechi zinazofuata," amesema Samatta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live