Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta ampa mchongo Msuva

94672 Msuva+pic Samatta ampa mchongo Msuva

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Casablanca, Morocco. Mshambuliaji wa Difaa el Jadida, Simon Msuva amesema Mbwana Samatta amefungua milango ya kucheza soka Ulaya.

Msuva alisema amejifunza kupitia Samatta baada ya kujiunga na Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England.

Alisema anatarajia idadi kubwa ya mawakala wataanza kuitupia jicho Tanzania kupitia jina la Samatta.

“Samatta amefungua njia kazi iliyopo ni jinsi gani ya kuitumia vizuri ili kufanikisha na kuitangaza nchi. Amefanya kazi kubwa kuisafisha kazi yetu ni kupita kwa uangalifu na malengo,” alisema Msuva.

“Samatta ameonyesha njia tangu akiwa African Lyon, Simba, TP Mazembe, Genk na Aston Villa tunatakiwa kufanya zaidi ya hapo ili kudhihirisha vipaji vyetu nchini,” alisema.

Msuva ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Difaa na ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatarajiwa kuuzwa mwishoni mwa msimu kutokana na kufanya vizuri katika Ligi ya Morocco, mashindano ya Afrika na timu ya Taifa.

Pia Soma

Advertisement
“Kweli nilikuwa niuzwe klabu ya Panathinaikos ya Ugiriki, lakini dili lilikwama baada ya klabu hiyo kushindwa kutoa fedha ambazo Difaa ilizokuwa inazihitaji,” alisema.

Msuva alisem anatarajia kujiunga na timu nyingine msimu ujao ingawa alikataa kuitaja klabu hiyo akidai bado ni mapema.

“Ni klabu ya Ulaya siwezi kusema ni mapema sana, ila nakuhakikishia kuwa mwisho wa msimu na pengine hata kabla ya mwisho wa msimu dili la kuondoka litakuwa limekamilika,” alisema winga huyo wa zamani wa Yanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz