Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta akubali mziki wa Morocco, awapongeza Watanzania

Samatta Morocco Samatta akubali mziki wa Morocco, awapongeza Watanzania

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa kikosi cha Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Samatta amesema Morocco walikuwa bora ndiyo maana wamepata kipigo cha mabao 2-0 juzi.

Stars ilipoteza pambano hilo la kutafuta nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akiandika katika ukurasa wake rasmi nyota huyo anayekipiga Klabu ya PAOK ya nchini Ugiriki ameandika; “Ni matokeo ambayo hatukupenda kuyapata lakini hatuna budi kukubali mpinzani alikuwa na mchezo bora.

“Tutautumia mchezo huu kurekebisha na kujifunza ili kufanya vyema katika michezo itakayofata. Asante wapenzi wa Soka wote mliojitokeza uwanjani.

“Nyinyi ni mashabiki mahiri sana. Tutarudi wakati ujao tukiwa na nguvu zaidi,“ aliandika Samatta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live