Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye yupo KRC Genk kwa mkopo anaweza kurejea muda wowote kwenye klabu yake ya Fenerbahce.
Samatta ambaye alijiunga na KRC Genk kwa mkopo wenye kipengele cha kusajiliwa moja kwa moja, amekuwa akikumbana na changamoto ya namba kwenye kikosi hicho ambacho hii ni awamu yake ya pili kukichezea.
Kitendo cha kutopata nafasi mbele ya Paul Onuachu, kimetafsiriwa na mtaalamu wa usajili nchini humo, Ekrem Konur kuwa kile kipengele chake kwenye mkataba wake wa mkopo kinaweza kisitekelezwe na badala yake anaweza kurudishwa Uturuki.
Samatta mwenye miaka 30 anamkataba na Fenerbahce hadi Juni 2024, kabla ya kuamua kurejea Ubelgiji mezani mwake alikuwa pia na ofa za Uarabuni lakini aliona kuwa bado anaweza kuendelea kucheza soka la ushindani.