Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta afungukia kipigo cha Misri

Samatta 681x454.jpeg Samatta afungukia kipigo cha Misri

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbwana Samatta nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Misri ni kipimo tosha katika kuelekea mashindano ya AFCON 2023.

Ikumbukwe kwamba Januari 7 2024 timu ya taifa ya Tanzania ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri baada ya dakika 90 ubao ulisoma, Tanzania 0-2 Misri.

Trezeguet alifunga bao la ufunguzi dakika ya 32 na bao la pili lilifungwa na Mohamed Salah dakika ya 73.

Samatta amesema: “Ulikuwa ni mchezo mzuri na wenye ushindani mkubwa kwa kuwa wapinzani wetu ni timu nzuri. Kucheza na timu ya Misri kwetu ni kipimo tosha kuelekea mechi za AFCON hasa ukizingatia Misri ina uzoefu na wachezaji wazuri,”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live