Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta aenziwa Genk, jezi yake yauzwa

Sdv Samatta Samatta aenziwa Genk, jezi yake yauzwa

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta ameendelea kuenziwa na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji kwa jezi yake maalum kuuzwa katika maduka ya timu hiyo.

Samatta ambaye ni Legend wa timu hiyo amewekwa katika kundi la wachezaji watano wa kikosi hicho waliowahi kupita na kufanya mambo makubwa.

Katika duka la kuuzia vifaa vya michezo la timu hiyo kuna jezi maalum iliyotengenezwa na kuuzwa katika duka hilo, moja ya jezi inayouzwa ni pamoja na jezi ya Samatta yenye picha yake akiwa anafunga kwa kichwa katika mechi ya Genk na Liverpool.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live