Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta achomoza kikosi Bora Afrika

Samatta Afrika.png Samatta achomoza kikosi Bora Afrika

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha na Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta ametajwa kwenye kikosi cha muongo (Miaka Kumi iliyopita) cha Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kikosi hiki kimechaguliwa na kutajwa baada ya kura zilizopigwa na mashabiki kwa njia ya mtandao.

Samatta ametajwa katika orodha hiyo iliyojumuisha wachezaji waliotamba kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrikakundia mwaka 2010 mpaka 2020.

Mshambuliaji huyo alifanya vizuri sana kwenye Michuano hiyo akiwa na wababe wa Lubumbashi-DR Congo TP Mazembe kuanzia mwaka 2011-2016, huku klabu hiyo ikitwaa Ubingwa wa Afrika msimu 2014/15

Baada ya mafanikio hayo, Mwaka 2015 Samatta alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika ‘CAF’ kwa wachezaji wa ndani, akitangulia na tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo pia.

Pia, mwaka huo wa 2015 alitajwa kwenye kikosi bora cha mwaka cha Barani Afrika kupitia Shirikisho la Soka Barani humo ‘CAF’.

Huyu ndiye mtanzania pekee kuwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara la Afrika.

Wachezaji wengine waliotajwa kwenye orodha ya Kikosi Bora cha Afrika cha muongo (Miaka Kumi iliyopita) ni Malinda Lango kutoka Uganda Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Wael Gomma, Ahmed Fatty, Hossam Ghaly, Hossam Ashour, Ali Maaloul, na Walid Soliman (Al Ahly-Misri).

Wengine ni Mshambuliaji kutoka Zambia Stopilla Sunzu (TP Mazembe) Percy Tau (Mamelodi Sundowns na Al Ahly pamoja na Kiungo Mshambuliaji kutokanchini Zimbabwe Khama Billiat (Kaizer Chief).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live