Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta, Novatus wasikilizia droo Europa

Samatta X Novatus Samatta, Novatus wasikilizia droo Europa

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wawakilishi wa PAOK ambayo anaichezea Mbwana Samatta huko Ugiriki na Shakhtar Donetsk ya Ukraine anapokipiga Novatus Dismas, wapo Nyon, Uswisi ambako leo, Jumatatu itachezeshwa droo ya hatua ya mtoano ya michuano ya Europa Conference League na Europa League.

Droo ya kwanza kuchezeshwa kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) itakuwa ya Europa League saa 9:00 alasiri huku ikifuatiwa na Europa Conference League saa moja baadaye.

Mkurugenzi wa Michezo wa Shakhtar Donetsk, Darijo Srna ametajwa kuwa Uswisi kwa ajili ya kufuatilia moja kwa moja mpinzani ambaye watakutana naye kwenye hatua ya mtoano ambayo itaanza kuchezwa Februari 15, 2024.

Shakhtar ambayo anaichezea Novatus imeangukia upande wa Europa League ambao una vigogo kwenye soka la Ulaya kama vile AS Roma na Liverpool baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi H la Ligi ya Mabingwa Ulaya, nyuma ya FC Barcelona na FC Porto.

PAOK ilimaliza kwa kishindo hatua ya makundi ya Europa Conference League baada ya kujikusanyia pointi 16 kwenye kundi G ambalo lilikuwa na Eintracht Frankfurt ya Ujerumani, inaonekana kuwa ngumu.­­­­­­

Chanzo: Mwanaspoti