Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta, Msuva kutua Stars kesho

Samatta Pic Data Samatta, Msuva kutua Stars kesho

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

NYOTA na nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta na Washasmbuliaji Saimon Msuva na Yohana Mkomola wanatarajiwa kuwasili kwenye kambi ya timu hiyo mapema kesho.

Taarifa kutoka Jijini Nairobi, Kenya ilipo kambi ya Stars zinaeleza kuwa nyota hao watatu watawasiri mapema kesho nchini humo tayari kwa kuungana na wenzao ambao wapo hapo kambini tangu Machi 13 mwaka huu.

Nyota hao walichelewa kufika kambini hapo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya klabu zao, Samatta Akiwa     Fenerbahce ya Uturuki, Msuva akiwa  Wydad Casablanca ya Morocco  na Mkomola akiwa Ingulets Petrove ya Ukraine.

Kikosi cha Stars kikiwa chini ya kocha mkuu Kim Poulsen kimeweka kambi nchini Kenya ambapo kilitarajia kucheza mechi mbili dhidi ya timu ya Taifa hilo 'Harambee Stars' lakini ilicheza mchezo mmoja Machi 15 na kupoteza kwa kufungwa bao 2-1 huku mechi nyingine iliyokuwa imepangwa kuchezwa Machi 18 ikifutwa kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulialiyeaga dunia Machi 17 mwaka huu.

Yote hayo ni kueleka kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika 'Afcon' dhidi ya Guinea ya Ikweta mchezo utakaokuwa wa marudiano kwani ule wa duru ya kwanza ulichezwa Novemba 15, 2019 na Stars kushinda 2-1 mabao ya Stars yakifungwa na Msuva dakika ya 69 na Salum Abubakar 'Sure Boy' dakika ya 90 huku lile la Guinea likifungwa na Pedro Obiang dakika ya 15.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz