Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samagoal yuko anga zingine kabisa Ulaya

32049 Pic+samata Samatta

Mon, 17 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Miaka ya 70’s kulikuwa kuna mtu anaujua sana mpira. Alikuwa akihangaika uwanjani.

Aliitwa kompyuta. Huyu si mwingine ni Sunday Manara ambaye anashikilia rekodi ya kuwa nyota wa kwanza wa Kitanzania kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Sunday ambaye ni baba wa msemaji wa Simba, Haji Manara alikipiga Uholanzi kunako klabu ya Heracles na kuondoka kwake nchini mwaka 1976 kulitokana na mgogoro ambao ulikuwepo Yanga.

Ni miaka 42 imeyoyoma tangu Manara alipoweka rekodi hiyo tamu na sasa tuna Golden Boy, Mbwana Samatta ambaye anaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania barani humo.

Mchezo wa soka ni kama mbio za vijiti vile kikipita kizazi kimoja kinakuja kingine kuendeleza pale ambapo waliopita waliishia.

Hata kama ataoondoka leo Samatta kwenye soka la ushindani ile rekodi yake ya 2016 itaendelea kukumbukwa maana ni mchezaji wa kwanza wa ukanda wa Afrika Mashiriki kushinda tuzo ya mchezo bora wa ndani kwa wachezaji wa Afrika.

Kipindi hicho aliweka rekodi hiyo kwa kufunga mabao saba yaliyomfanya kuibuka mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika na yaliisaidia timu yake aliyokuwa akiichezea TP Mazembe kuchukua ubingwa huo.

Samatta ambaye Wabelgiji wamempa jina la Samagoal kutokana na uwezo wake wa kuifungia mabao klabu yake ya KRC Genk msimu huu, amekuwa moto wa kuotea mbali, amefunga mabao 11 akitumia dakika 1,331.

Kabla ya michezo ya Jumamosi na Jumapili, hivi ndivyo anavyokimbizana na mastaa wengine wakubwa barani Ulaya kwa kupachika mabao kwenye zile Ligi Kubwa na bora barani humo zikiwemo, EPL, Bundesliga, La Liga, Ligue 1 na Eredivisie.

Ligue 1 - Sala/Mbappe (12)

Vichwa viwili vinavyoonekana kuwa kwenye viwango vya hali ya juu msimu huu wa 2018/19 kwenye Ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 ni Emiliano Sala wa Nantes na Kylian Mbappé wa PSG ambao kila mmoja amefunga mabao 12.

Mbappe ametumia jumla ya dakika 837 katika michezo tisa kufunga mabao hayo na kutengeneza mengine manne kwa hiyo anawastani wa kufunga bao moja kwenye kila baada ya dakika 70.

Sala ametumia jumla ya dakika 1109 kufunga idadi hiyo ya mabao, mshambuliaji huyo ametengeneza mabao mawili.

Eredivisie - De Jong (14)

Mshambuliaji wa PSV Eindhoven ya Uholanzi, Luuk de Jong amepachika mabao 14, ana mabao mawili zaidi ya mastaa wa Ufaransa, Emiliano Sala wa Nantes na Kylian Mbappé wa PSG, kinara huyo wa mabao kwenye Eredivisie anawastani wa kufunga bao moja kwenye kila baada ya dakika 96.

JPL - Santini /Samatta (11)

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayeichezea KRC Genk na Ivan Santini wa Anderlecht kila mmoja amefunga mabao 11, Ligi Kuu Ubelgiji.

Samatta, 25, na Santini wamefunga mabao hayo kwenye michezo 18 ya JPL.

Ndani ya michezo hiyo, Samatta mbali na kufunga mabao 11 lakini pia ametengeneza bao moja huku kwa Dimata akiwa na mabao matatu ya kutengeneza.

La Liga - Messi/ Stuani (11)

Lionel Messi ametumia jumla ya dakika 1051 kufunga mabao hayo kwenye La Liga, mshambuliaji huyo anawastani wa kufunga kila baada ya dakika 96. Messi ametengeneza mabao manane msimu huu kwenye La Liga.

Cristhian Stuani upande wake na Girona yake amefunga mabao hayo kwenye michezo 15 ya La Liga, mshambuliaji huyo wa Kiruguay anawastani wa kufunga bao moja kwenye kila baada ya dakika 93.

Bundesliga - Jovic (10)

Mshambuliaji wa Frankfurt ya Ligi Kuu Ujerumani, Luka Jovic ndiye kinara wa mabao kwenye Bundesliga kwa sasa akiwa na mabao 10 ambayo ametumia dakika 818 kuyafunga, Jovic ana wastani wa kufunga kwenye kila baada ya dakika 82.

Serie A - Piatek (11)

Genoa ya Italia wanamtambo mmoja tu wa mabao ambao ni Krzysztof Piatek aliyeifungia timu hiyo mabao 11 kwenye Serie A na kuwa kinara wa mabao mbele ya mastaa wengine wakali kwenye Ligi hiyo ya Italia kama vile, Cristiano Ronaldo wa Juventus mwenye mabao 10.

Wengine ni Ciro Immobile wa Lazion mwenye mabao 10, Fabio Quagliarella wa Sampdoria, Mauro Icardi wa Inter Milan na Francesco Caputo wa Empoli kila mmoja akiwa na mabao manane.

EPL – ‘Mo’ Salah/ Aubameyang (10)

Washambuliaji wengine wa Kiafrika Mohamed Salah wa Liverpool na Pierre-Emerick Aubameyang wa Arsenal wote wana idadi sawa ya mabao, Ligi Kuu Englanda ambayo ni maarufu kama EPL.



Chanzo: mwananchi.co.tz