Kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga @salehjembefacts amesema wachezaji wanaogopa mechi za dabi kwa sababu ya presha ya mchezo huo na kusababisha wachezaji kukosa ubunifu.
Amesema wachezaji ambao hawajawahi kucheza dabi kama jean Baleke wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri tofauti na wachezaji ambao wameshazoe kucheza mechi hizo.
"Uoga wa wachezaji unapunguza ubunifu, Mayele alivyokuja mechi ya kwanza tulimuona alifunguka akapata bao, hivyo ndivyo navyoona kwa Baleke, atakuwa hana hofu sana kwa vile dabi hajaijua vizuri kwa hiyo atafunguka.
"Kadri dabi unavyoizoea ndivyo mchezaji anakuwa muoga, anaogopa kuharibu kwenye mechi hiyo kwa sababu lawama ni nyingi," amesema Jembe.
Simba itavaana na Yanga Jumapili kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC utkaochezwa saa 11:00 jioni uwanja wa Benjamin Mkapa Dar.