Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salah amtaja Nunez kama mchezaji mwenye kasi zaidi Liverpool

Salah Nunez Salah amtaja Nunez kama mchezaji mwenye kasi zaidi Liverpool

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, amemtaja mchezaji mwenye kasi zaidi klabuni hapo.

Mmisri huyo, ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa mawinga wenye kasi zaidi duniani, anaamini Darwin Nunez ndiye mwanasoka mwenye kasi zaidi kwenye klabu hiyo kwa sasa.

Wachezaji wa Liverpool walikuwa wakiulizwa maswali mbalimbali yanayohusu michezo ya Olimpiki wakati wakirekodiwa video zitakazotumika kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na ndipo Salah alipochomekea jambo hilo.

Nunez alijiunga na Liverpool kutoka Benfica mwaka 2022.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay amefunga mabao 33 katika mechi 96 alizocheza klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live