Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salah aisimamisha Man City Anfield

Salah Record Liver Mfungaji wa goli la Liverpool, Mohammed Salah

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kuisimamisha klabu ya Manchester City baada ya kuifunga bao moja kwa bila katika mchezo uliopigwa katika dimba la Anfield.

Klabu ya Manchester City ambayo ilikua haijapoteza mchezo hata mmoja msimu huu imekubali kipigo cha bao moja kwa bila kutoka kwa vijogoo wa Merseyside huku wakiendelea kubaki nafasi ya pili na alama zao 23.

Bao pekee la mchezo huo liliwekwa kimiani na mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Misri Mohamed Salah ambaye ameendeleza moto wake baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya katikati ya wiki dhidi ya Rangers.

Klabu ya Liverpool ambayo imeanza ligi vibaya msimu huu huku ikiwa imeshinda michezo miwili tu kabla ya mchezo dhidi ya City na baada ya ushindi wa leo inakua ushindi wa tatu na kuwafanya kufikisha alama 13 huku wakisogea kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 10 mpaka ya 8 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Liverpool pia wamefanikiwa kua timu ya kwanza msimu huu kuifanya Manchester City kumaliza mchezo bila kupata bao lolote huku mshambuliaji wake matata Earling Haaland akishindwa kufurukuta kabisa katika mchezo huo.

Manchester City wanapoteza mchezo wao wa kwanza msimu huu katika michuano yote huku pia wakweka rekodi ya kumaliza mchezo bila kufunga bao lolote huku ikiwa ni rekodi mbaya zaidi msimu huu kwa vijana hao wa Pep Guardiola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live