Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salah aipa Liverpool alama tatu muhimu

WhatsApp Image 2023 05 04 At 09.jpeg Mohamed Salah alifunga bao pekee la Liverpool

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao la Nyota Mmisri, Mohamed Salah dakika ya 39 kwa penalti limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumatano Uwanja wa Anfield.

Penalti hiyo ilitolewa baada ya Darwin Nunez kuangushwa kwenye boksi na Issa Dip na kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 59 katika mchezo wa 34, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi nne na Manchester United ambayo pia ina mechi mbili mkononi.

Kwa upande wao Fulham baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 45 za mechi 34 pia nafasi ya 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: