Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salah aing'arisha Afrika EPL

Salah Mo 120 Winga wa Liverpool, Mohamed Salah

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ushindi wa Liverpool wa mabao (2-0) dhidi ya Everton ,Juzi Jumamosi Mohamed Salah anakuwa mchezaji wa kwanza wa Kiafrika kufunga magoli 145 katika Ligi Kuu ya Uingereza hii ni baada ya kufunga mabao mawili peke yake .

Tangu kuanza kwa mwaka huu 2023 tayari amehusika kwenye magoli zaidi ya 30+ kwenye ligi kuu Uingereza EPL

31 Mechi

19 magoli

12 assist

Mbali na hapo Salah amefanikiwa kufikisha mabao 201 kwenye maisha yake ya soka la kulipwa akicheza kwenye ligi kuu mbali mbali [ Magoli ya Ligi kuu tu]

Mechi 13 zilizotangulia akiwa katika uwanja wa Anfield amefunga au kutoa assist kwenye mechi zote (Asipokufunga basi atatoa assist)

Idadi ya magoli ya jumla aliyofunga kwenye uwanja wao Anfield ni 104 hii ni sawa na Kenny Dalglish na Steven Gerrard (Magoli ya jumla Anfield)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live