Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salah aiepushia Misri aibu ya kufungwa na Msumbiji

Salah Aibu Salah aiepushia Misri aibu ya kufungwa na Msumbiji

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Mkwaju wa penalti wa dakika za majeruhi wa Mohamed Salah uliepusha aibu ya Misri dhidi ya Msumbiji katika mechi ya kwanza ya Kundi B kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 baada ya timu hizo kutoka sare ya 2-2.

Mabao ya kipindi cha pili ya haraka haraka kutoka kwa Witi na Clesio yaliwapa Mambas matumaini ya kuandikisha ushindi wa kwanza kabisa wa Afcon.

Lakini ndoto zao zilikatizwa wakati Domingos Macandza alipomshika Mohamed, na Salah kufanikisha sare hiyo

Kwingineko bao la haraka la Victor Osimhen la kusawazisha liliiokoa Nigeria dhidi ya kushindwa katika mechi kati yao na Equatorial Guinea katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1.

Cape Verde iliisumbua Ghana kwa bao la dakika za lala salama na kuwashinda kwa 2-1 ili kuongoza Kundi B katika Kombe la Mataifa ya Afrika 2023.

Ratiba ya mechi za leo:Jumatatu 15 Januari

Kundi C: Senegal vs Gambia, Charles Konan Banny Stadium, Yamoussoukro (14:00)

Kundi C: Cameroon vs Guinea, Yamoussoukro (17:00)

Kundi D: Algeria vs Angola, Stade de la Paix, Bouake (20:00)

Chanzo: Bbc