Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salah, Mane na Mahrez chama moja, Andre Onana, Kudus chama jingine

Salah X Maqneee Salah, Mane na Mahrez chama moja, Andre Onana, Kudus chama jingine

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mikikimikiki ya Afcon 2023 inashirikisha mastaa wa maana wanaocheza soka kwenye ligi kubwa mbalimbali huko duniani, ambao watashuka Afrika kwenda kukipiga kwenye timu zao za taifa.

Fainali hizo zitakata utepe leo Jumamosi kwa mechi kali baina ya wenyeji Ivory Coast dhidi ya Guinea-Bissau. Mambo ni moto.

Masupastaa kama Mohamed Salah na Victor Osimhen watakuwa na shughuli pevu ya kuongoza vikosi vyao kwenye mchakamchaka wa kubeba ubingwa wa timu hiyo ambapo fainali yake itapigwa Februari 11.

Morocco inapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa fainali hizi za Afcon 2023, huku pia kura zikizitaja Senegal, Algeria, Ivory Coast, Egypt na Nigeria kwenye uwezekano wa kunyakua taji hilo.

Katika kuelekea kuanza kwa fainali hizo, hiki hapa Kikosi cha Kwanza kinachoundwa na mastaa wakali waliopo kwenye fainali hizo za Ivory Coast.

Yassine Bounou, aka Bono, amekuwa mahiri sana golini na atakuwapo kwenye fainali za Afcon 2023 akiidakia Morocco, ndiye anayepata nafasi kwenye kikosi hiki kwa upande wa makipa.

Kwa sasa anaidakia Al-Hilal ya Saudia na ukuta wake kwenye kikosi cha pamoja, upande wa kulia atakuwa staa wa Achraf Hakimi, kushoto Ramy Bensebaini na mabeki wa kati ni Nayef Aguerd na Edmond Tapsoba.

Beki huyo wa kushoto anaichezea Borussia Dortmund na Algeria, wakati beki wa kati Tapsoba anaichezea Bayer Leverkusen na Burkina Faso. Aguerd ni West Ham United na Morocco.

Staa wa Napoli na Cameroon, Andre-Frank Zambo Anguissa na mkali wa Tottenham Hotspur na Senegal, Pape Matar Sarr watatengeneza kombinesheni matata kabisa kwenye sehemu ya kiungo.

Kwenye safu ya ushambuliaji kumesheheni mastaa wenye vipaji vya hali ya juu, akiwamo mkali wa Liverpool na Egypt, Mo Salah na straika wa Napoli na Nigeria, Osimhen.

Mastaa wa zamani wa Ligi Kuu England, wanaokipiga Saudi Arabia kwa sasa, Sadio Mane wa Senegal na Riyad Mahrez wa Algeria wanakamilisha kikosi hicho matata kabisa cha wakali wa maana Afcon 2023.

Kipa wa Manchester United na Cameroon, Andre Onana atakuwa kwenye benchi baada ya kufanya makosa mengi tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Old Trafford, huku fowadi wa West Ham United na Ghana, Mohammed Kudus na straika wa Chelsea na Senegal, Nicolas Jackson wamekosa nafasi kwenye kikosi hicho cha kwanza na kuunda kikosi kingine cha pili, chenye wakali wa maana pia.

Chanzo: Mwanaspoti