Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakho ashinda Tuzo ya Bao Bora CAF

Sakho Tuzo Bao Bora Sakho ashinda Tuzo ya Bao Bora CAF

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Simba ambaye ni raia wa Senegal, Pape Ousmane Sakho amefanikiwa kushinda Tuzo ya Bao Bora la Mwaka katika Tuzo za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Julai 21, 2022.

Tuzo hizo zimetolewa Rabat Nchini Morocco ambapo Sakho alikuwa akiwania nafasi hiyo dhidi ya Gabadinho Mhango wa Orlando Pirates na Zouhair El Moutaraji wa Wydad Athletic Club.

Sakho alilifunga bao hilo wakati #Simba ikishinda 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas mchezo wa Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam, Februari 13, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live