Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakho aibua vita mpya

Pape Ousmane Sakho Shoot Sakho aibua vita mpya

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba kinaendelea kujifua kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuvaana na Polisi Tanzania katika mechi ya Ligi Kuu Bara, huku kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Pape Ousmane Sakho akiibua vita mpya baada ya wikiendi iliyopita kufunga mabao mawili na kubanana na nahodha wake, John Bocco kila mmoja akiwa na mabao tisa.

Simba itavaana na Polisi inayopambana kuepuka kushuka daraja, ikiwa ni wiki chache tangu iishushe Ruvu Shooting kwa kuifumua mabao 3-0 katika pambano lililopigwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa Sakho akifunga mabao mawili akitokea benchi na kuibua vita hiyo tamu kikosini.

Sakho amekuwa hana nafasi katika kikosi cha kwanza, ameibuka mwishoni kama ilivyokuwa msimu uliopita aliomaliza na mabao sita, ameanzisha vita ya ufungaji ndani ya Simba, lakini akiwa na kibarua cha mechi zilizosalia kuona kama anaweza kumpiku kinara Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 16 hadi sasa.

Sakho amesaliwa na bao moja tu kwa sasa kumfikia kinara wa mabao wa timu hiyo, Moses Phiri mwenye 10, huku Saido Ntibazonkiza naye akiwa na idadi kama hiyo japo manne alitoka nayo Geita Gold akiwa sambamba na Phiri nyuma ya Mayale.

Kama Sakho ataendelea kupewa nafasi ya kufunga mabao mengi zaidi ana nafasi ya kupiku Phiri na kumaliza kama kinara wa mabao wa klabu hiyo, kwani Mzambia huyo kwa sasa hapewi nafasi na kocha Robertinho.

Ila mambo yakienda hovyo, huenda Simba ikajikuta kwa msimu wa pili mfululizo ikishindwa kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora, kwani msimu uliopita ilibebwa na George Mpole aliyekuwa Geita Gold akifunga 7, akimzidi Mayele aliyemaliza na 16 kama aliyonayo kwa sasa ligi ikielekea ukingoni.

Simba itamaliza msimu kwa pambano dhidi ya Coastal Union litakalopigwa Juni 9 badala ya Mei 28 kutokana na mabadiliko madogo yaliyofanywa na Bodi ya Ligi Kuu Bara ili kupisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na USM Alger zitakazopigwa Mei 28 na Juni 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: