Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakho afurahia Banda kurejea uwanjani 'nilimisi asist zake'

Pape Sakho Na Banda Sakho afurahia Banda kurejea uwanjani 'nilimisi asist zake'

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pape Othman Sakho amesema anafuraha kubwa kumuona Jerry wake, Peter Banda anarejea dimbani tayari kuitumikia klabu yao ya Simba SC.

Sakho ameyasema hayo wakati yeye pamoja na wachezaji wenzao walipokuwa kwenye mazoezi ya kujiandaa dhidi ya mchezo wao wa Kombe la Azam Federation Novemba 28, 2023 dhidi ya Coastal Union.

"Amekuwa muda kwa mrefu, nilimmisi sana. Nilimisi asist zake, nilikuwa nikimtia moyo maana alikuwa anajisikia vibaya kuona sisi tunacheza wakati yeye hawezi kucheza kutokana na majeraha.

"Sasa yupo fiti ameshakata kitambi kama unavyomuona, kwa kweli nafurahi kumuona amerudi," alisema Sakho.

Banda ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi mitatu tangu apate majeraha Novemba 29, 2022 katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Singida Big Stars, anatarajia kurudi rasmi kwenye mechi za ushindani wiki ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live