Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Pape Sakho ameweka wazi kuwa lengo lao kama timu ni kwenda kuhakikisha wanapambana na kupata ushindi ugenini nchini Guniea katika mchezo wao dhidi ya Horoya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika.
Sakho amesema, kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo huo na yupo tayari kuhakikisha anapigania timu kupata matokeo mazuri ugenini.
Akizungumzia kukosekana kwa kiungo mshambuliaji Saido Ntabazonkiza, Saido amesema alitamani angekuwepo kikosini kutokana na ubora na uzoefu wake lakini siku zote majeruhi sio kitu kizuri kwa mchezaji.
"Maandalizi yetu ni mazuri, malengo yetu ni kushinda ugenini, tutapambana ili kufanikisha hilo. Tunajua haitakuwa mechi rahisi, tutakuwa ugenini lakini tupo tayari kwa mpambano na mashabiki wetu tunawaomba watuombee tukatimize malengo yetu," amesema Sakho.