Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Yanga, Fei Toto kuwakilishwa na mawakili wa Morrison

Fei Oneee Sakata la Yanga, Fei Toto kuwakilishwa na mawakili wa Morrison

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kimeumana! ndivyo unavyoweza kusema kuhusu sakata la mkataba wa kiungo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na uongozi wa Yanga, ambapo leo Ijumaa kiungo huyo ameripoti kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuitikia wito wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuhusu shauri lake la kuvunja mkataba akiambatana na mawakili waliowahi kumsimamia Morrison.

Desemba 23, mwaka jana Fei Toto aliwasilisha barua ya kuvunja mkataba na Yanga baada ya kurudisha kiasi cha shilingi Milioni 112 na mshahara wa miezi mitatu kuendana na matakwa ya kimkataba na kuwaaga mashabiki wa timu hiyo Jumamosi ya Desemba 24.

Hatua hii ambayo ilipingwa na Yanga ambao wanasisitiza bado Feisal ni mchezaji wao mpaka Mei 2024.

Morrison aliwahi kusimamiwa na mawakili katika sakata lake la kutoka Yanga kwenda Simba ambapo walishinda. Ilidaiwa Morrison alisaini Simba wakati bado ana mkataba na Yanga.

Chanzo chetu cha kuaminika kilicho karibu na Fei Toto kimesema kuwa, leo Ijumaa Fei Toto anataitikia wito kwa kutua katika ofisi za TFF ambapo atawakilishwa na mawakili walioshughulikia kesi ya Bernard Morrison wakati akiwa na mgogoro wa kimkataba na Yanga kabla ya kuibuka mshindi wa kesi hiyo.

“Ni kweli Fei Toto amewasili Tanzania kutoka Dubai kwa ajili ya kusikiliza shauri la kesi ya mkataba wake na Yanga ambayo inatarajiwa kusikilizwa kesho (leo) Ijumaa kwenye Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF.

“Jambo la kushangaza ni kuwa Fei Toto atawakilishwa na mawakili ambao walikuwa wakisimamia kesi ya Morrison kuhusiana na sakata la mkataba wake na Yanga wakati anajiunga na Simba ambayo Morrison alishinda.

“Sambamba na mawakili hao Fei Toto pia ataongozana na wazazi wake wote wawili kwa lengo la kuhakikisha kama shauri hilo halitamalizwa kesho (leo), basi wazazi hao watabaki kuendelea ‘kumlinda’ mtoto wao hadi kieleweke.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live