Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Mshambuliaji, Yanga mchukueni huyu..!

Matheo Anthony X Mzize Sakata la Mshambuliaji, Yanga mchukueni huyu..!

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga kwa sasa inatakiwa kupambana kumrejesha kwenye timu mshambuliaji wa klabu ya Mtibwa Matheo Anthony, Matheo Anthony aliwahi kucheza katika klabu ya Yanga akiwa kijana mddogo sana chini ya kocha Hans baada ya kusajiliwa kutokea Zanzibar.

Matheo Anthony wakati yuko Yanga alikuta na na changamoto ya kutopata nafasi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa washambuliaji bora na wenye uzoefu kama Donald Ngoma, Hamis Tambwe na Obrey Chirwa

Kwenye Nbc premier league Matheo Anthony amefunga mabao matatu kwenye ligi, Mabao mawili akifunga dhidi ya Simba, Kwasasa yuko katika kiwango bora sana na tayari ameshaonyesha ukomaavu katika ligi kuu Tanzania bara

Yanga toka ameondoka Mayele jicho kubwa kwa washambuliaji wa kati timu inamtegemea Clement mzize, Musonda na Konkoni bado hawajaonyesha makali yakuweza kuibeba klabu ya Yanga kwenye safu ya ushambuliaji, Kama watamsajili Matheo Anthony wakiunga na Clement Mzize Yanga itakuwa na safu bora ya ushambuliaji

Chanzo: www.tanzaniaweb.live