Rais wa muda wa Shirikisho la soka la Hispania Pedro Rocha ameitisha mkutano wa kipekee na wa dharura hapo kesho ili kutathmini hali inayoendelea kufuatia sakata la busu la mdomoni lililotokea katika sherehe za Kombe la Dunia la Wanawake.
Mkutano huo unalenga kupata suluhisho la kinachoendelea au kukubaliana hatua za kuchukua.
Hadi sasa Luis Rubiales ambaye ndiye Rais wa shirikisho hilo amekataa kujiuzulu, hata hivyo FIFA imemsimamishwa kazi kwa siku 90 kupisha uchunguzi.
Rubiales ameahidi kujitetea hata mbele ya mahakama ,na kusisitiza kuwa busu lake la mdomoni kwa mchezaji Jenni Hermoso lilikuwa la kawaida na kitu ambacho alikifanya kwa ridhaa ya mchezaji huyo.