Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Mayele na Yanga limefikia hapa

Fiston Kalala Mayele Life Sakata la Mayele na Yanga limefikia hapa

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mazungumzo kati ya Yanga na Striker wao, Fiston Mayele yamefikia sehemu nzuri sana kuhusu Mchezaji huyo kuendelea kuwatumikia Wananchi kwa mkataba mpya.

Mkataba wa mchezaji huyo na Yanga umebakia mwaka mmoja na mpaka sasa Mayele amepata ofa za Kaskazini zikituma ofa ya kumnunua pia na za Kusini zikihitaji huduma yake.

Taarifa za uhakika kwa mujibu wa vyanzo vyangu ni kuwa Uongozi muhimu wa Yanga umekubali kumpatia Tsh 40M ili kuendelea kusalia katika klabu hiyo kuelekea msimu mpya.

Kuna taarifa za chini chini kuwa Mayele alipewa ofa na Yanga ya Tsh 28M ili abakie JANGWANI kwa misimu miwili ila Striker huyo alikataa, kwaiyo dili hilo limekamilika kwa asilimia kubwa Fiston Mayele kubaki Yanga.

Kutokana na hilo Striker huyo ataanza kulipwa Tsh 40M baada ya msimu 2023/24 kutamatika, hivyo ataendelea kupokea Tsh 16M mpaka mkataba wake wa awali utakapo tamatika kwa mujibu wa Mazungumzo.

Fiston Mayele yupo kwenye mipango ya Yanga kuelekea 2023/24, Yanga hawatamuachia Mchezaji yoyote katika kipindi hiki ambaye yupo kwenye mipango ya timu kuelekea msimu mpya kwa mujibu wa Viongozi muhimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live