Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Lawi na Simba, mbivu na mbichi kujulikana leo TFF

Lawi X Magori Sakata la Lawi na Simba, mbivu na mbichi kujulikana leo TFF

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inakutana pale kwenye ofisi za TFF zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam kupitia mashauri kadhaa yaliyopo mezani kwao.

Pamoja na mashauri mengine, Kamati hiyo pia itajadili sakata la beki Lameck Lawi ambaye Simba inasema ilimsajili kihalalaki wakati Coastal Union ikikomaa kwamba hakuna dili hilo.

Lawi anatajwa kusajiliwa Simba huku waajiri wake Coastal Union wakikiri kuwa bado ni mchezaji wao hivyo timu ambayo imemnunua mchezaji huyo imewasilisha malalamiko juu ya usajili wake.

Akizungumza nasi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Said Soud alisema ni kweli leo watakutana kujadili mashauri yote yaliyowasilishwa kwenye kamati yao.

"Kikao kitafanyika kesho (leo) lakini siwezi kuthibitisha ni kesi gani zipo mezani kwa sababu huwa tunakutana nazo siku ya tukio, kuhusiana na Lawi na mimi nimesikia kama ulivyosikia wewe," alisema na kuongeza;

"Kamati yetu ni sawa na wanasheria mahakamani kesi ambazo hawajawahi kuzisimamia wanakutana nazo maakamani tofauti na zile ambazo zimeshasikilizwa na kupangiwa tarehe nyingine."

Soud alisema wanakutana kujadili ikiwa ni utaratibu wao kukutana mara baada ya usajili kufanyika ili kupitia pingamizi zilizopo.

“Dosari kwenye suala la usajili huwa hazikosekani, sisi tunakutana kuangalia wapi kuna shida ili mambo yakae sawa,” alisema.

MSIKIE MAGORI

Licha ya Lawi kuendelea kusalia nchini wakati Simba ipo Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crescentius Magori amekiri kuwa huyo ni mchezaji wao wanasubiri uamuzi wa kamati baada ya kupeleka malalamiko huko.

Alisema ni mchezaji wao kwani walifanya taratibu zote za malipo kwa ajili ya kumnunua lakini ghafla mambo yakaenda tofauti lakini hilo sasa lipo chini ya kamati husika, hivyo hawezi kulizungumzia sana.

"Msimamo wetu sisi Simba ni kwamba Lawi ni mchezaji wa Simba japo tunasubiri maamuzi ya kamati na kama yatatoka tofauti tutakata rufaa ili kuhakikisha jambo hili linafanyika kwa haki." alisema Magori.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: