Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Lawi na Simba; Said Soud aondolewa kwenye chumba cha maamuzi

Said Soud Ds.jpeg Said Soud (kulia)

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Said Soud ametolewa nje baada ya mwanasheria upande wa Simba SC kuomba Mwenyekiti huyo atolewe nje.

Said Soud ametolewa nje kwenye shauri la kesi la mchezaji Lameck Lawi baada ya Mwenyekiti huyo kutajwa kuwa ni mwanachama na shabiki wa Coaster Union.

Said Soud ametoka nje amewaachia wajumbe waendelee na shauri hilo linalosikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwenye ofisi za TFF, zilizopo Ilala Dar es Salaam.

Coastal na Simba zimeingia kwenye mgogoro wa kumgombania beki Lameck Lawi Simba ikimtangaza kama mchezaji wao na Coastal ikisema mchezaji huyo hajauzwa bado ni mali ya Coastal.

Klabu ya Coastal Union yenye maskani yao mkoani Tanga ina viongozi mbalimbali na wanachama (TFF).

◉ Wallace Karia ›› Mwanachama Coastal.

◉ Steven Mguto ›› Mwenyekiti Coastal.

◉ Said Soud ›› Mwanachama Coastal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live