Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Kagoma na Yanga, mwanasheria aibua jipya tena

Kagoma Saaa Yusuph Kagoma

Fri, 13 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

"Wadau wa michezo wengi Tanzania wanaongozwa na hisia na hawataki ukweli, hoja za msingi ni hizi hapa;

1. Kanuni zetu haziruhusu mchezaji kusaini mkataba na vilabu 2, lakini Yusuph Kagoma amesaini mikataba 2 na anakiri hilo, je hili ni sawa kwa mujibu wa kanuni zetu?

2. Hakuna taasisi imekaa chini na kubatilisha mkataba mmoja wapo kati ya aliyoisaini mchezaji, hii inamaana gani?

3. SFG wanasema Yanga ilichelewa kufanya malipo kwa siku 5, je kanuni ya 12bis (3) ya kanuni za FIFA za uhamisho na hadhi za wachezaji (RSTP) ya 2024 inasemaje kuhusu ucheleweshwaji wa malipo?

Swali la msingi: Kama mnadai timu inayowahi kumsajili mchezaji ndiyo ina haki na mchezaji, ni wakati gani kanuni ya 41(13) inayozuia mchezaji kusaini mkataba na klabu zaidi ya moja itafanya kazi!? Logic

NB: Nitasimama upande wa sheria na kanuni sio upande wa hisia." amesema hayo Mwanasheria wa klabu ya Yanga SC Simon Patrick.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live