Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Feisal, Yanga inshu bado ngumu

Feisal Salum Fei Toto'' Feisal Salum

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikao cha dakika 60 cha kusikiliza shauri la kiungo Faisal Salum dhidi ya Waajiri wake Yanga SC kimemalizika na nyota hugo ameondoka katika ofisi za TFF.

Mwanasheria wa Feisal akiwa kwenye gari na Feisal kabla ya kuondoka kwenye Ofisi za TFF amewaambia Waandishi wa Habari kuwa bado hawajapata majibu wala hawajaona mwanga wowote kuhusu sakata hilo na kwamba hawezi kujua kama Feisal atarejea Yanga ama la na kusisitiza wanaojua hilo ni TFF.

Aidha Mwanasheria huyo amesema kwa sasa mchezaji huyo atakua akipatikana Zanzibar na kusisitiza kwamba hajui chochote kama atarejea Yanga au la, pia alipoulizwa Feisal ni Mchezaji wa Timu gani kwa sasa amejibu “bado, siwezi kuongea lolote”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live